The House of Favourite Newspapers

Basata Yamzuia Steve Kuwa Msemaji wa Shirikisho la Wasanii

0

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limetoa maelekezo kwamba Steve Mengele aliyeteuliwa kuwa Msemaji wa Shirikisho la Wasanii asianze kufanya kazi hiyo kwanza hadi pale Baraza litakapofanya maamuzi.

 

Haya yamebainika baada ya BASATA kuitisha kikao leo tarehe 23 2022 kwenye ofisi za Baraza kwa lengo la kupata kiini cha mgogoro huo na kukitafutia ufumbuzi ambapo baada ya kuusikia upande wa shirikisho BASATA ilijiridhisha kwamba Bodi ya Utendaji ya Shirikisho hilo ilifanya kikao chake na kufanya uteuzi huo.

 

“Baraza linaendelea kufanyia kazi taarifa zilizowasilishwa na Viongozi wa Shirikisho pamoja na kufanyia kazi hoja za Wajumbe waliohudhuria kikao hicho na litatoa uamuzi wake mapema iwezekanavyo ambapo kuhusu Msemaji Steven Mengele Baraza linatoa maelekezo asianze kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo hadi hapo itakapoamuliwa na Baraza” — imeeleza taarifa ya BASATA

Leave A Reply