The House of Favourite Newspapers

Basata Yaungana na Kampuni ya Chapride Kunogesha Tuzo za TMA, Watu 1500 Kusafiri Bure

0

 

Kuelekea kilele cha Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) zitakazotolewa April 29, 2023 katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), limeungana na Kampuni ya Chapride ili kuzinogesha tuzo hizo.

Katibu Mtendaji wa Basata, Dr. Kedmon Mapana amesema Kampuni ya Teksi Mtandao ya Chapride, imejitolea kuwasafirisha BURE watu 1500, kwenda na kuondoka katika Ukumbi wa Super Dome kushuhudia event ya utoaji wa tuzo hizo.

 

Dk. Mapana amesema kwa mwaka huu kutakuwa na jumla ya tuzo 52 zitakazotolewa usiku huo na kuwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura.

Mbali na hayo, Dk. Mapana amesema tuzo za mwaka huu zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni Tuzo ya Heshima, Tuzo Maalum na Tuzo za Jumla.

Pia ameipongeza @chapridetz kwa kukubali kuwaunga mkono Watanzania watakaohudhuria siku hiyo kwa kutoa ofa ya kuwasafirisha bure kabisa wakati wa kwenda ukumbini na hata wakati wa kurudi.

Leave A Reply