The House of Favourite Newspapers

Bashungwa: Lazima Tusanifu Makaravati na Madaraja kwa Umakini

0

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema iko katika hatua za mwisho kuanza kujenga madaraja mawili ya Chakwale na Nguyami Wilayani Gairo ili kuwaondolea kero ya muda mrefu wananchi wa maeneo hayo.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa anabainisha hayo wakati wa ziara yake Mkoani Morogoro ya kukagua miundombinu ya Barabara ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya MHE Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtaka Waziri huyo kufika kusiko fikika ili kutatua kero za wananchi hususan miundombinu ya Barabara.

Akiwa Wilayani Gairo amewaambia wananchi kuwa Serikali chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan imekwisha ridhia ujenzi wa madaraja hayo mawili ya Chakwale na Nguyami ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza Juni 2024, Daraja la Chakwale likiwa na urefua wa mita 80 na lile la Nguyami likiwa na urefu wa mita 100, lengo ni kuwaondolea wananchi kero ya kupoteza Maisha wa eneo hilo na mali zao.

Aidha, Waziri Bashungwa amemuagiza Mtendaji wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROAD), kufanya usanifu wa kina wa madaraja hayo ili yawe ya viwango na yaje kutumika pia wakati watakapoamua kujenga Barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahamed Shabiby ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kujali wananchi katika kuwaletea maendeleo yao kwa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Miundombinu na kuweka bayana kuwa hakuna Serikali iliyotoa fedha nyingi kwa Sekta ya Miundombinu kama Serikali ya awamu ya sita.

Kwa upande wake meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro amesema tayari washafanya upembuzi akinifu kuanza ujenzi wa barabara ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa wilaya ya Gairo na wilaya ya kilindi mkoani Tanga.

Aidha waziri bashungwa akiwa Wilayani Kilosa amemtaka mkandarasi anayejenga Barabara ya kutoka Rudewa hadi Kilosa mjini kwa Kiwango cha lami kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha Barabara hiyo ifikapo Aprili 22 mwaka huu kwa kuwa hana kisingizio tena kwani fedha alizokuwa anazidai shilingi Bilioni 4 amekwisha lipwa.

Leave A Reply