The House of Favourite Newspapers

Bastola, Gobole Vyakamatwa Katika Palanja la Polisi – Video

0

POLISI  Mkoa wa Mbeya inamshikilia Amani Mpindule (68) Mkazi wa Lualaje kwa tuhuma za kumiliki silaha bunduki aina ya Gobole bila kuwa na kibali.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo Julai, 25, 2020 katika Hifadhi ya Mwenje – Ruaha iliyopo Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya katika msako wa pamoja kati ya Jeshi la Polisi na Askari wa mbuga za taifa za wanyama (TANAPA).

 

Pia Julai 25, 2020, Mtaa wa Iyela, Iyunga, jijini Mbeya,  walikamata Bastola yenye namba ya usajili TGT.10582 / PT.809E aina ya TAURUS ikiwa na risasi moja ndani ya magazine iliyotengenezwa nchini Brazil.

 

Wakati huohuo, Polisi imewatia mbaroni watu wanne kwa tuhuma za wizi kwa njia ya mtandao kwa kutumia laini na mashine za makampuni ya simu.  Watu hao ni Issa Said, Jonathan Fikiri Tanganyika, Obedy Mwaselle na William Salvatory Jonas.

 

Kufuatia tukio hilo, polisi imewataka wananchi kuwa makini pindi wanapofanya usajili wa laini zao za simu ili kuepuka kadi zao kutumika kusajili laini za watu wengine.

 

Leave A Reply