The House of Favourite Newspapers

Batuli asikitikia Figisu ndoa ya Rayuu

0

11007850_412854112229544_460047070_n1Staa wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’.

Stori: Mayasa Mariwata

STAA wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amesema miongoni mwa vitu vinavyomnyima furaha kipindi hiki ni ndoa ya msanii wa filamu, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ambayo inadaiwa kuvunjika.

Akibonga machache na paparazi wetu juzikati, Batuli alisema anawashangaa wanao shabikia ndoa hiyo kuyumba, mbaya zaidi wengi wao ni wanawake ambao huenda nao siku moja yakawafika.

“Niliona jambo la heri Rayuu kuolewa, sasa hizi figisu zinazoibuka zinanikosesha amani kabisa, kikubwa afuate taratibu za dini kuhusiana na talaka hiyo,” alisema Batuli.

Leave A Reply