The House of Favourite Newspapers

Bayern Yarukia Dili la Rabiot

Kiungo wa Paris St. Germain, Adrien Rabio.

BAYERN Munich inatajwa kumwania kiungo wa Paris St. Germain, Adrien Rabiot. Barcelona kwa muda mrefu sasa imekuwa inatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili kiungo huyo.

Rabiot, amebakiza miezi sita katika mkataba wake na PSG, amegoma kusaini mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo.

Uwezekano sasa mkubwa ni staa huyo ataondoka bure PSG na ataongea masuala ya mshahara na timu itakayomuhitaji. Taarifa zinasema kuwa Rabiot alishamalizana na Barcelona, ambao atajiunga nao baada ya msimu huu kumalizika.

Bayern Munich inasemekana inataka kutibua dili hilo kwa kupeleka dau PSG ili wamnase katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili. PSG nayo inataka kumuuza Rabiot katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili wa mwezi Januari.

Comments are closed.