The House of Favourite Newspapers

Ihefu Yafanya Mabadiliko Ya Jina Kutambulika Kama Singida Black Stars

0

Klabu ya lhefu Fc iliyohamisha makazi yake kutoka Mbarali mkoani Mbeya na kwenda Mkoani Singida imefanya mabadiliko ya jina lake kutoka IHEFU SPORTS CLUB na sasa itatambulika kama SINGIDA BLACK STARS SPORTS CLUB

Taarifa ya Mkurugenzi wa Utawala wa klabu hiyo, Muhibu Kanu imebainisha kuwa nia na malengo ya kubadilisha jina hilo ni kuiunganisha timu na wananchi wote wa Mkoa wa Singida.

Taratibu zote za usajili wa jina hilo tayari zimesha kamilika kwa kufuata miongozo, kanuni na taratibu zote za Nchi, TFF na BMT.

“SINGIDA BLACK STARS SC tumelenga katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wa nchi yetu ili kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao kupitia vipaji walivyo navyo” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

“Ni imani yetu kubwa kwambwa tutaendelea kushirikiana na wadau wote kila mmoja kwa nafasi yake kuendeleza mpira wa Nchi yetu.” — SINGIDA BLACK STARS SC

Leave A Reply