The House of Favourite Newspapers

Jamaa Ataka Kumuua Mama’ke Na Kumtupa Buza, Mama Aokotwa Akiwa Hoi – Video

0


Mapya yanazidi kuibuka kufuatia tukio la kijana aliyefahamika kwa jina la Clemence Mahela mkazi wa Yombo Matangini kwa Mbembe jijini Dar es Salaam kudaiwa kumuua mama yake na kwenda kuutupa mwili wake msituni.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni ndugu wa mwanamke aliyefanyiwa ukatili huo, anaeleza kuwa walipatwa na hofu baada ya kuuona mtuhumiwa akiwa anafua nguo za ndugu yao zikiwa na damu majira ya usiku.

Hali hiyo ilifanya watoe taarifa kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ambao walimfungia mtuhumiwa kusubiri polisi wafike ambapo akiwa ndani, alijaribu kujiua kwa kujichoma na bisibisi tumboni.

Leave A Reply