Bela Adai Uzazi Haujamuachisha Muziki

Isabela Mpanda ‘Bela’

Mwanamuziki wa Kundi la Scorpion Girls, Isabela Mpanda ‘Bela’ baada ya kimya kingi ameibuka na kudai kuwa uzazi haujamuachisha muziki bali ameshajipanga na mwaka mpya atatoka na wimbo ambao amemshirikisha msanii mwenzake, Rashida Wanjara.

 

Akipiga Stori na Showbiz, Bela alisema kuwa baada ya kukaa na kuona kuwa wenzake kwenye Kundi la Scorpion Girls hawako ‘siriasi’, wao wameamua kurudi na kuliendeleza wakiamini wanao uwezo wa kulifanya lishaini upya.

 

“Unajua kuzaa kwangu hakuwezi kuniachisha muziki, ni kitu ninachokipenda ambacho kipo kwenye damu na sasa mimi na Rashida tutashangaza wengi, kwani wimbo tutakaoutoa hakuna ambaye hatausifia,” alisema Bela. Wanamuziki waliokuwa wanaunda Kundi la Scorpion ni pamoja na Baby Madaha, Miriam Jolwa ‘Kabula’ Bela na Rashida.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Loading...

Toa comment