The House of Favourite Newspapers

Bella na Madaha ni kweli wanaishi kisagaji?

bella-na-madaha-1

WAREMBO wanaowakilisha Kundi la Scorpion Girls, Baby Joseph Madaha na Isabela Mpanda ‘Bella’ walitinga ndani ya mjengo wa Global Publishers juzikati, wakazungumza na Gazeti la Ijumaa sanjari na Global TV Online.

Wamefunguka mambo mengi ikiwemo skendo ya usagaji iliyokuwa ikiwatafuna kwa muda mrefu, tujiunge nao hapa chini:

Ijumaa: Kwanza mtuambie kuhusu ujio wenu mpya, tumesikia mna wimbo mpya. Idea ikoje?

Baby Madaha: Ngoma yetu inaitwa Marioo, tumeona tuwaimbe wanaume wanaopenda kulelewa maana wanaume wa aina hii wapo wengi mjini.

 bella-na-madaha-2

Baby Joseph Madaha na Isabela Mpanda  wakiwa Global TV.

Ijumaa: Inasemekana Bella umemuimbia mpenzi wako Kalama, katika hii ngoma kuna ukweli?

Bella: Hapana sisi tulitaka tu kuleta ujumbe kwa wale mamarioo, lakini sikumuimbia mtu.

Ijumaa: Kitu gani unachokikumbuka kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wako, Kalama.

Bella: Kitu cha kwanza ambacho nakumbuka alikuwa anampenda mtoto wangu na alikuwa ananipiga sana. Kitu kingine, alikuwa ananiridhisha kimahaba kwa kweli.

 bella-na-madaha-3

…Katika pozi na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.

Ijumaa: Nini kiliwafanya muachane?

Bella: Mwisho ulifika sababu kila kitu kina mwanzo na mwisho, mwisho ulifika ndiyo maana tukaachana.

 

Ijumaa: Inasemekana memba wenzenu wa Scorpion kina Jini Kabula na Jack Pentzel mmewafukuza, kwa nini?

Baby Madaha: Scorpion ilizaliwa mwaka 2008, tulikuwa kwenye bethidei. Ikaenda sasa mambo ya ugomvi wa hapa na pale yalitokea lakini baadaye nikarudi tena, nikawashawishi tukaanza kulisongesha lakini baadaye tena Jini Kabula akasema ameshawishiwa na mchungaji amrudie Mungu, aimbe gospo. Tukamruhusu.

Toka hapo tukabaki mimi na Bella, tunalisongesha mpaka sasa. Bado pia tunaangalia, wale waliojitoa, wakirejea tutawaangalia kama tukiona inafaa, tunawarudisha.

 

Ijumaa: Mna uongozi unawasimamia?

Baby: Hatuna ile management kamili lakini tunaye mama Loraa, yeye aliamua tu kutupa njia ya kuelekea kwenye mafanikio lakini bado hatuna meneja rasmi, mama yetu ameamua tu kutusaidia.

 bella-na-madaha-4

Ijumaa: Bella kuna habari inasambaa kwenye mitandao kwamba Jack Pemba ndiye anayekuweka mjini ni kweli?

Bella: Yule ni mshkaji wangu, tumekutana naye nje ya nchi tukapiga picha lakini baadaye ndio yakaibuka ya kuibuka.

Jack Pemba amenifanyia mambo mazuri sana, nilipokwenda Uganda kwenye shoo, alitupokea vizuri sana hivyo atabaki kuwa mshkaji.

 bella-na-madaha-5

…Wakiwa katika pozi na Mtangazaji wa Global TV Online, Calvin Shayo.

Ijumaa: Baby Madaha tulisikia una mpenzi mwarabu Oman? Ni kweli?

Baby Madaha: Watu tu wanasema, hamna mtu Oman, mahusiano yangu mimi nilishayaweka ‘private’.

 

Ijumaa: Iliwahi kudaiwa kuwa unajihusisha na skendo ya usagaji kwa kumgeuza Bella ‘mkeo’, ukamdatisha hadi akamuacha mpenzi wake, hili likoje?

Baby Madaha: Ulikuwa ni uzushi tu, hawakuwa na hoja. Unajua wanasema hivyo kwa sababu hawajawahi kumuona mpenzi wangu.

Ijumaa: Una mpenzi lakini?

Baby Madaha: Ndio yupo hapahapa Tanzania lakini sina mpango wa kumuonesha kwenye vyombo vya habari.

Ijumaa: Imeelezwa kwamba ndiye amekupangia nyumba Mbezi.

Baby Madaha: Sijawahi kupangiwa nyumba na mwanaume. Mimi ni mtafutaji balaa. Mimi siyo marioo wa kike, anipangie kama nani? Amenioa?

Mimi bado natafuta mchumba, hakuna ambaye anaweza kujimilikisha.

Ijumaa: Bella wewe ndio umefika kwa Mzungu wako Mr Rolex sasa hivi, au bado unaweza ukammwaga?

Bella: Mimi kwanza boyfriend wangu haitwi Mr Rolex, siyo jina lake. By the way sio kwamba nimefika, mimi kila kitu ni surprise, ninaweza nikasema ndio mume wangu halafu asiwe.

Mimi mwenyewe kichaa, kama kuna kitu kaniudhi nampiga chini mchana kweupe.

Ijumaa: Si unajua kuna Ukimwi?

Bella: Yeah si ‘najiprotect’, mimi mwenyewe ni mama, najua namna ya kujilinda.

Ijumaa: Baby Madaha wewe ni mtu wa bata sana, unafikiri unaweza kumaliza kreti ngapi za bia?

Baby Madaha: Bia kwangu mimi ni starehe. Inategemea nimeenda sehemu gani, nafikiri ni bora kunywa bia kadiri iwezekanavyo. Nakunywa zaidi nikiwa naangalia muvi.

Ijumaa: Huoni kama unaweza kunywa halafu ukafanyiwa kitu mbaya?

Baby Madaha: Hamna mimi nakunywa maeneo ya jirani, nahakikisha pia nipo salama.

Ijumaa: Bella umewahi kuvuta bangi?

Bella: Sijawahi kuvuta ila nimekunywa bia karibu zote duniani labda pengine nimebakisha aina 7 tu.

Ijumaa: Baby unazungumziaje wimbi la wasanii kuingia kwenye madawa ya kulevya?

Baby Madaha: Ile ni hali ya kutojikubali kutokana na gemu kukataa, ni ngumu sana kuwarudisha watu ambao wameshaingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya. Ni tatizo, wote tunapaswa kulipiga vita.

Comments are closed.