The House of Favourite Newspapers

Belle 9: Sitasahau nilivyotendwa kimapenzi

0

belle 9MWANAMUZIKI anayefanya poa ‘always’ kwenye gemu la Muziki Bongo, akitamba kwa sasa na remix ya Wimbo wa Burger Movie Selfie, Abednego Damian ‘Belle 9’ amefunguka kuwa katika maisha yake hata kuja kusahau namna alivyotendwa na msichana aliyempenda mno hata kuwa na malengo naye kwenye maisha yake, msikie akistorisha kiaina na Burudani Mwanzo Mwisho (BMM).

BMM: Ilikuwa lini hiyo ulipotendwa?

Belle 9: Kipindi nilipomaliza sekondari, halafu mbaya zaidi baada ya huyu msichana kunitenda akawa anapita kitaani kwetu nilipokuwa nakaa na washikaji mara kwa mara, so ilikuwa inaniuma sana.

BMM: Washikaji hawakuwa wanakucheka?

Belle 9: No! Wengi walikuwa wananitia moyo na kuniambia nitakuja kupata atakayenipenda.

BMM: So ilikuwaje ukamsahau na sasa yuko wapi?

Belle 9: Dah! Ilichukua muda sana, lakini baadaye nilipata msichana mwingine tuliyependana. Ukweli ni kwamba sitamsahau, kuhusu yuko wapi sifahamu kwa kweli.

Leave A Reply