The House of Favourite Newspapers

Benki Kuu (BoT) Yakanusha Kutoa Sarafu ya Sh. 3,000

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba mwezi Julai, mwaka huu, (2019)  ilitoa sarafu ya kumbukumbu ya visiwa vya Dokdo yenye thamani ya shilingi 3,000.

Katika taarifa kwa umma, benki hiyo imesema habari hizo si za kweli na kwamba sarafu hiyo siyo mali ya benki hiyo, haijatolewa na benki hiyo na haijawahi kuingia mkataba na kampuni yoyote kutoa sarafu hiyo.

Comments are closed.