The House of Favourite Newspapers

Benki ya Absa Yatoa sh Milioni 45 Kudhamini Absa Dar City Marathon

0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga ( wa pili kulia ) akizungumza jijini Dar es Salaam leo  wakati akitangaza udhamini wao wa shs milioni 45 katika mbio za  Absa Dar City Marathon.Wengine kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Britam Insurance, Leoncia Makobo, Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, Godfrey Mwangungulu, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni wa Bima ya Alliance Life Assurance, Jawa Masomo na na Katibu wa The Runners, Scola Kisanga.

WATANZANIA wameshauriwa kulinda afya zao Kwa kushiriki mbio na mazoezi ya viungo kwani afya ni mtaji muhimu katika shughuli za uzalishaji mali.

Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga wakati akizungumzia udhamini wa Absa katika mbio za kilomita 21 za Absa Dar City Marathon, zinazotarajiwa kutimua vumbi jijini humo jumapili wiki hii.

Bwana Aron alisema Benki ya Absa kwa kutambua kuwa  afya ni mtaji mkubwa sana Kwa wafanyakazi, wateja na Kwa jamii ya watanzania na kuwa bila ya kuwa na afya njema shughuli za kiuchumi haziwezi kwenda kadri zinavyotakiwa benki yao imekubali kutoa udhamini wa mbio hizo wenye thamani ya shs milioni 45.

Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, waandaaji wa Dar City Marathon ,Godfrey Mwangungulu (wa pili kulia), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga.

“Kama Absa tunajisikia furaha sana kuungana na waandaaji wa Dar City Marathon tukiwa wadhamini wakuu wa mbio hizi tukitoa udhamini wa kiasi cha shs milioni 45 ambazo pia zikiwa na lengo la kuisaidia jamii kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

“Natoa wito kwa  watanzania, wateja wetu kujitokeza Kwa wingi kushiriki mbio hizi, mtu akiwa anafanya mazoezi akiwa anakimbia, anajenga afya na hapo hapo anapata utajiri wake.

“Baada ya mbio hizi tutaungana na Runners Club kwenda katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Ili kukabidhi vifaa vitakanyosaidia jamii wakiwemo watoto kupambana na  magonjwa yasiyoambukiza”, alisema Bwana Aron.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga ( kulia ), Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Klabu ya The Runners, Godfrey Mwangungulu, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni wa Bima ya Alliance Life Assurance, Jawa Masomo, Meneja Masoko wa Britam Insurance, Leoncia Makobo na Katibu wa The Runners, Scola Kisanga, wakionyesha fulana zitakazovaliwa siku ya mbio  za Absa Dar City Marathon

Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Habari  Klabu ya  The Runners waandaaji wa mbio hizo, Godfrey Mwangungulu alitoa shukurani kwa Absa pamoja ma wadhanini wengine kwa kudhamini mbio hizo ambazo zaidi ya Watu 3000 watashiriki akisema pamoja mambo mengine zitasaidia kutangaza vivutio vya utalii vya Jiji la Dar es Salaam kwani zitapita katika mitaa mashuhuri ya jiji hilo.

“Tunaungana na majiji mengine sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa sehemu ya historia kwenda kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii katika Jiji letu la Dar es Salaam, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mbio hizi kufanyika katikati ya jiji, natoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kwa pamoja na mbio hizo pia kuna burudani mbalimbali zimeandaliwa zitakazofanyika katika ziwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam”, alisema.

Mbio za Absa Dar City Marathon zitajumuisha mbio za kilomita 21, mbio za kilomita 10 na mbio za kujifurahisha za kilomita 5 ambazo zawadi mbalimbali zitatolewa zikiwemo pesa tasilimu kwa mshindi wa kwanza hadi wa 10 kwa wanawake na wanaume.

 

 

 

Leave A Reply