Benki ya CRDB Yaingia mkataba na TFF kudhamini Kombe la Shirikisho
Benki ya CRDB imeingia mkataba rasmi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo itatoa zaidi ya shilingi Billioni tatu kudhamini
Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania maarufu
Kombe la FA.
Rais wa TFF Wallace Karia amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa mkataba huo utakuwa ni wa miaka mitatu.
Amesema kutokana na CRDB kudhamini Kombe la FA sasa litaitwa
CRDB Bank Federation Cup.