The House of Favourite Newspapers

Meli Unayoweza Kununua Chumba kwa Mabilioni Yatua Kwa “Royal Tour” Dar

0

The World-Residences at Sea, moja ya meli kubwa za kifahari duniani na ambayo imekuwa ikizunguka dunia kwa miaka 20 sasa ipo Dar es Salaam, Tanzania, muda huu unaposoma makala haya na imetia nanga Jumamosi Machi 30, 2024.

Meli hiyo ni tofauti na nyingine nyingi duniani kwani haina abiria (passengers) bali ina matajiri takribani 400 ambao ni wamiliki (residences) walioununua vyumba vyenye ukubwa mbalimbali katika meli hiyo na hupanda kila mwaka kwenda kuzunguka maeneo mbalimbali ya dunia safari inayochukua miezi mitatu kwa mzunguko mmoja.

Chumba kimoja hugharimu hadi Dola Milioni 2 (takribani TZS Bilioni 4.5) ambapo nyumba kamili ndani ya meli hiyo yenye vyumba vitatu na mambo mengine ya kifahari huuzwa kwa Dola Milioni mpaka 15 (Zaidi ya TZS Bilioni 30).

 

Kazi kubwa ya kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya “Tanzania: The Royal Tour”iliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa mambo yaliyowavutia mabilionea wengi waliokuja na meli hiyo iliyoanzia kutua Mafia, Zanzibar na sasa iko Dar mpaka kesho jioni. Baadhi ya watalii hao wameruka kwa ndege kwenda kutalii maeneo mengine kama Serengeti, Ngorongoro na Hifadhi ya Nyerere.

 

“Mimi binafsi nimekuwa nikivutiwa na Rais Samia na alipoingia tu madarakani niliandika makala moja nzuri kumtambulisha duniani na katika ulimwengu wa utalii. Nikavutiwa zaidi alipofanya filamu kuitangaza nchi. Nchi yenu ina kila kitu mnapaswa kuitangaza zaidi,” anasema, Alain St. Ange, Waziri wa zamani wa Utalii, Anga na Bandari wa Visiwa vya Seychelles, alipokutana baada ya kushuka kwa muda kwenye meli hiyo akiwa mmoja wa watu waliokuja nayo na kufanya mazungumzo na Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania juu ya namna ya kushirikiana nao jinsi ya kuitangaza zaidi Tanzania na kuleta meli zaidi nchini na kupanua utalii wa fukwe, visiwa na meli.

Leave A Reply