The House of Favourite Newspapers

DCB Yaunga Mkono Serikali Mapambano Dhidi ya Ugonjwa wa Corona

0
Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Mazingira wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dk. Khalid Massa ( wa pili kushoto), akitakasa mikono yake katika moja ya vifaa 100 vya kutakasia mikono vyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 30 vilivyotolewa na Benki ya Biashara ya DCB vitakavyowekwa katika vituo mbalimbali vya daladala na mwendokasi jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa hatari wa homa ya mapafu wa Corona (Covid-19). Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za wizara jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa. Wa tatu kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daudi Msasi.
Mfamasia Mkuu  wa Serikali, Daudi Msasi (katikati), akitakasa mikono yake katika moja ya vifaa 100 vya kutakasia mikono vyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 30 vilivyotolewa na Benki ya Biashara ya DCB vitakavyowekwa katika vituo mbalimbali vya daladala na mwendokasi jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa hatari wa homa ya mapafu wa Corona (Covid-19).  Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Afya Mazingira wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dk. Khalid Massa.
Mfamasia wa Wizara ya Afya, Neema Nagu  (katikati), akitakasa mikono yake katika moja ya vifaa 100 vya kutakasia mikono vyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 30 vilivyotolewa na Benki ya Biashara ya DCB .
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa (kushoto), akiweka kitakasa mikono katika chupa katika hafla ambayo DCB ilikabidi vifaa vifaa 100 vya kutakasia mikono vyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 30.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa (wa tatu kushoto), akikabidhi baadhi ya vitakasa 100 nyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 30 vilivyotolewa na benki hiyo vitakavyowekwa katika vituo mbalimbali vya daladala na mwendokasi jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na ugonjwa hatari wa homa ya mapafu wa Corona (Covid-19). 

 

 

 

Leave A Reply