The House of Favourite Newspapers

Benki ya Dunia Yaitaka TZ Kutowabagua Wanafunzi Wajawazito

0

Benki ya dunia imeishinikiza serikali ya Tanzania kuanzisha mfumo wa elimu kwa wanafunzi wanaokatiza masomo yao kutokana na sababu kama vile ujauzito.

 

Ikuzungumza katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi, benki hiyo imesema kwamba inafuatilia kwa karibu maswala yote yanayoendelea nchini Tanzania na kwamba itaendelea kushirikiana na taifa hilo katika maswala ya elimu.

 

Akizungumza katika mkutano huo mkurugenzi wa benki ya dunia anayeiwakilisha Marekani Dkt. Jennifer “DJ” Nordquist amesema benki hiyo inavutiwa na mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali ya Magufuli katika utoaji wa elimu ya bure kwa shule za msingi na sekondari.

Leave A Reply