The House of Favourite Newspapers

BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA TAWI LAKE JIPYA MBAGALA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza jambo katika hafla hiyo ya uzinduzi wa tawi jipya la benki ya KCB eneo la Mbagala.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na viongozi wa KCB wakizindua rasmi tawi hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya KCB, Zuhura Muro naye akizungumza jambo katika hafla hiyo.

 

 

BENKI ya KCB Tanzania imefanya uzinduzi wa tawi lake la 14 lililopo Mbagala jijini Dar es Salaam, tawi ambalo limezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa kiserikali.

 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mh, Felix Lyaniva, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke-  Mh. Abdallah Chaurembo, Mbunge wa Temeke, Issa Mangungu, Kamanda wa Polisi Wilaya ya  Temeke ACP Emmanuel Lukula, Ndugu Diwani wa kata ya Mbagala- Jumanne Kambangwa, Ndugu Viongozi na maafisa mbalimbali wa Serikali, Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa KCB Bank.

KCB Bank imewezesha miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kutokana na rasilimali za KCB Group (strong balance sheet). Miradi hiyo ni kama Barabara ya Msata hadi Bagamoyo, Ujenzi wa Terminal Three (3) JNIA, jengo la One stop Centre TPA na Emergency Laboratory Building (Ofisi ya Raisi, Makumbusho) kwa kutaja tu michache.

 

 

Katika hotuba yake mwenyekiti alisema, “Ndugu mgeni rasmi natumaini unakumbuka vizuri mwaka 2017 uliitikia wito wa kuwa mgeni rasmi kwenye warsha ya tujiajiri iliyokutanisha wanawake zaidi ya 1500 hapa jijini Dar es Salaam. Leo nina furaha kurudisha mrejesho kuwa baada ya kutambua mahitaji ya kifedha ya wanawake wajasiriamali, KCB Banki imeshazindua “tujiajiri Women Account” amabayo inawawezesha kuweka akiba na kupata mikopo kwa masharti mepesi na rafiki. Ulitupa changagmoto nasi tukaifanyia kazi.”

Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa Tawi hilo la Mbagala ni sehemu ya jitihada za kuweza kufikia wateja wao wengi lakini pia kutanua wigo wa huduma za kibenki. Aliendelea  kusisitiza kuwa Mbagala ni moja ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu jijini Dar es Salaam vilevile kuna uwepo wa biashara ndogo, za kati na zile kubwa ambazo zinajumuishwa viwanda, usafirishaji, elimu na kadhalika na hivyo kuamini kwamba  tawi hilo litakidhi mahitaji ya kifedha kwa wateja wao wote katika eneo hilo na maeneo ya jirani.

 

 

Aliendelea  kuwakaribisha wakazi wote wa Mbagala  kutumia tawi hilo kwa huduma zao za kibenki na kufahamu zaidi faida zitokanazo na kuwa mteja wa KCB Bank ikiwemo mikopo, akaunti za akiba zenye faida lukuki, mtandao mkubwa wa ATM zaidi ya 962 Afrika mashariki.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa KCB, Cosmas Kimario alisema benki hiyo inaunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kuboresha huduma  ili kuendana na kasi ya mabadiliko na ukuaji wa uchumi.

 

 

 

Vilevile Mkurugenzi Mtendaji aliendelea kusema, kipindi cha kota ya kwanza ya 2018 benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi Bilion 3.6/- benki imeweza kuthibiti madeni chechefu (NPL) kufikia asilimia 7% kiwango ambacho ni kizuri katika utendaji wa kibenki.

 

 

KCB Bank imeahidi kuendelea kuboresha huduma na kusogeza karibu na wateja wao kwa kupitia njia za kidigitali kama vile simu za mkononi, mtandao wa intaneti pamoja na mawakala na hivyo  uboreshaji huo siyo tu utarahisisha upatikanaji wa huduma zao bali pia utaongeza idadi ya wananchi wanaofikiwa na huduma za kifedha (financial inclusion).

 

 

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji,  alipongeza KCB benki  katika shughuli zao za kusaidia jamii, hususani kwakuwa mstari wa mbele kwa kuwainua wanawake kupitia programu ya TUJIAJIRI, pia kwa udhamini wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania kuonesha nia ya kutaka kuinua sekta ya michezo, alisema “serikali inafurahishwa kuona kwamba mnainua jamii kwa misaada mbalimbali hasa kupitia sekat muhimu ya afya elimu, mazingira na wajasiriamali.

 

 

Aliongeza kwakusema, “nimefurahi kusikia kuwa utendaji wa Benki ya KCB ni mzuri, wenye faid na kiwango cha kuridhisha. Nimefurahi kusikia  kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2013-2017) KCB bank imefanya jitihada kubwa ikiwa ni pamoja  kuwa mlipaji mzuri wa kodi. Takwimu zenu zinaonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano (2013-2017) mmelipa jumla takribani shilingi bilioni arobaini (40) ikiwa kama corporate tax na kodi nyinginezo. huu ni mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu.”

 

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda.
KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.

 

 

Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki

Comments are closed.