The House of Favourite Newspapers

Benki ya NBC Ilala Yawafunfa Wajasiriamali

0
Meneja Ukuzaji Biashara wa Benki ya NBC Bw Isdory Sebastian (Kushoto) na Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Bi Sapiencia Masaga (Katikati) wakikabidhi cheti ushiriki wa mafunzo ya biashara, elimu ya fedha na mikopo kwa mmoja wa wajasiriamali Bi Sara Mrisho (Kulia) wakati wa semina fupi ya mafunzo ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Benki hiyo ikilenga kuwaandaa wajasiriamali hao waweze kutumia vema mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na manispaa hiyo.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam hii leo wameendesha mafunzo ya biashara, elimu ya fedha na mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali vijana, wanawake na walemavu waliopo katika Manispaa hiyo ikilenga kuwaandaa ili waweze kutumia vema mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na manispaa hiyo.

 

Meneja Ukuzaji Biashara wa Benki ya NBC Bw Isdory Sebastian (Kushoto) na Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Bi Sapiencia Masaga (Katikati) wakikabidhi cheti ushiriki wa mafunzo ya biashara, elimu ya fedha na mikopo kwa mmoja wa wajasiriamali Bi Najma Yusuph (Kulia) wakati wa semina fupi ya mafunzo ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Benki hiyo ikilenga kuwaandaa wajasiriamali hao waweze kutumia vema mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na manispaa hiyo.

 

Akizungumza kwenye mafunzo hayo yaliyowakutanisha pamoja wajasiriamali zaidi ya 400, Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Bi Sapiencia Masaga pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa jitihada hizo, alisema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa wajasiriamali hao kutumia vyema mikopo wanayoipata kutoka serikalini na halmashuri za jiji hilo ili kujikwamua kiuchumi kulingana na malengo ya mikopo hiyo.

 

Meneja Ukuzaji Biashara wa Benki ya NBC Bw Isdory Sebastian (Kushoto) na Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Bi Sapiencia Masaga (Katikati) wakikabidhi cheti ushiriki wa mafunzo ya biashara, elimu ya fedha na mikopo kwa mmoja wa wajasiriamali Bi Mwahija Rashidi (Kulia) wakati wa semina fupi ya mafunzo ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Benki hiyo ikilenga kuwaandaa wajasiriamali hao waweze kutumia vema mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na manispaa hiyo.

 

“Licha ya jitihada kubwa inayofanywa na halmashauri zetu kwa kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali vya vijana, wakina mama na walemavu bado tumekuwa hatupati matokeo mazuri sana kwasababu wengi wa walengwa wamekuwa wakishindwa kutumia vema mikopo husika na matokeo yake wanashindwa kufikia malengo na zaidi wanashindwa kufanya marejesho. Tunawashukuru NBC kwa kuwa mafunzo haya yanalenga kuondoa hiyo changamoto,’’ alisema.

 

Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Bi Sapiencia Masaga akizungumza na washiriki wa semina fupi ya mafunzo ya biashara, elimu ya fedha na mikopo iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Benki na Benki ya NBC ikilenga kuwaandaa wajasiriamali hao waweze kutumia vema mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na manispaa hiyo.

 

Kwa upande wake Meneja Ukuzaji Biashara wa Benki ya NBC Bw Isdory Sebastian alisema benki hiyo imeshirikiana na halmashauri ya Manispaa ya Ilala katika kutoa mafunzo hayo ili kujenga uelewa wa kutosha kuhusu usimamizi bora wa kifedha, umuhimu wa bima mbalimbali ikiwemo za afya na biashara pamoja na namna bora ya kutunza akiba zao waweze kuendesha shughuli zao kitaalamu ili waepukane na hasara zinazoweza kukwamisha ustawi wa biashara zao.

 

Maofisa wa Benki ya NBC wakitoa huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo usajili wa akaunti kwa washiriki wa semina fupi ya mafunzo ya biashara, elimu ya fedha na mikopo iliyoandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Benki na Benki ya NBC ikilenga kuwaandaa wajasiriamali hao waweze kutumia vema mikopo na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali pamoja na manispaa hiyo.

“Katika mafunzo hayo benki ya NBC tumejitahidi sana kuhakikisha walengwa wanajengewa uelewa wa kutosha ili sisi kama benki tusiishie tu kuwahifadhia fedha zao wanapokopeshwa na hizi halmashauri bali pia tuwasaidie kuhakikisha hiyo mikopo inakuwa na tija kwa pande zote yaani halmashauri na wajasiriamali.’’

“Tunawashukuru sana manispaa ya Ilala tungependa na Halmashauri nyingine pia waige mfano huu kwasababu mikopo hii inahitaji elimu sahihi kwa walengwa ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini na zaidi pia waweze kurejesha hizo fedha ili zitumike kuwakopesha wahitaji wengine,’’ alisema.

 

Wakizungumza kwenye mafunzo hayo, wajasiriamali Bw Iddy Kaziulaya na Bi Bahati Angetile walisema mafunzo hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwajengea uwezo wa kibiashara kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakishindwa kuendeleza vema mikopo hiyo kulingana na malengo kusudiwa hali inayochangiwa na kukosekana kwa elimu ya kutosha katika uendeshaji wa shughuli zao.

 

“Changamoto kubwa nayoiona kwasisi wanufaika wa hii mikopo ni kwamba wengi wanakopa kabla hawajawa na hata wazo la biashara matokeo yake pale tu wanapopatiwa fedha zinaishia kwenye mipango kabla ya utekelezaji wa mradi. Tunashukuru kupitia mafunzo haya wengi tutasaidiwa kufahamu namna ya kujinasua kwenye changamoto hii,’’ alisema Bw Kaziulaya.

NA MWANDISHI WETU

Leave A Reply