The House of Favourite Newspapers

Benki Ya NBC Yawafunda Wastaafu Watarajiwa Dar, Moro, Mtwara Na Zanzibar

0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa wakati wa semina ya Watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika taasisi za serikali na mashirika binafsi iliyoandaliwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.

 

 

Watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika taasisi za serikali na mashirika binafsi wameaswa kuweka mikakati thabiti ya matumizi bora ya rasilimali fedha sambamba na kupata elimu sahihi kuhusu huduma za kifedha na uwekezaji wa miradi sahihi ili waweze kuona matunda ya mafao yao pindi wanapostaafu.

Baadhi ya maofisa wa benki ya NBC tawi la Morogoro wakiongozwa na Meneja wa tawi hilo Bi Sophia Mwombela (Kulia) wakifuatilia semina ya Watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika taasisi za serikali na mashirika binafsi iliyoandaliwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo. Wengine ni Meneja biashara NBC Morogoro, Joseph Boaz (Kushoto) na Meneja mikopo NBC makao makuu Bi. Mtenya Cheya (Katikati).

 

 

Wito huo umetolewa na viongozi waandamizi wa Benki ya NBC katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Mtwara na Zanzibar walipopata fursa ya kuzungumza na wastaafu hao watarajiwa kwenye Semina ya siku mbili iliyoandaliwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo.

Ofisa Masoko wa Benki ya NBC Tawi la Mtwara Bw Stephen Ngerezi (Kushoto) akielezea huduma za benki hiyo kwa mmoja wateja alietembelea banda la benki hiyo wakati wa semina ya Watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika taasisi za serikali na mashirika binafsi iliyoandaliwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) mkoani Mtwara na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo.

 

 

Akizungumza kwenye semina hizo jijini Dar es Salaam na Morogoro, Meneja Mikopo kutoka Benki ya NBC Mtenya Cheya amewaasa watumishi hao kuheshimu na kutunza fedha katika taasisi zinazoaminika sambamba na kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato kwa kufuata ushauri madhubuti kutoka kwa wataalamu.

Meneja wa benki ya NBC tawi la Mtwara Bw Emmanuel Mseti akizungumza na wastaafu watarajiwa wakati wa semina ya Watumishi wanaotarajiwa kustaafu katika taasisi za serikali na mashirika binafsi iliyoandaliwa na mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) mkoani Mtwara na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki hiyo.

 

 

“Benki ya NBC tumejipanga kuwasaidia wastaafu watarajiwa na wale waliokwisha staafu na ndio sababu pamoja na kushiriki kwenye semina za mafunzo kama hizi pia tumekuwa na mikakati na huduma bora kwa wastaafu ikiwemo kutoa mikopo inayozingatia mahitaji yao,’’ alisema.

Baadhi ya wastaafu watarajiwa Zanzibar wakifuatilia semina hiyo.

 

 

Aidha Bi Mtenya alisema katika Juhudi za kuwakwamua wastaafu benki ya biashara ya taifa (NBC) imepania kuongeza nguvu zaidi kwenye  huduma maalum kwa wastaafu watarajiwa.

“Benki ya NBC tuna bidhaa maalumu kwaajili ya wastaafu watarajiwa, tuna mikopo, akaunti maalum lakini pia tunafundisha biashara ambazo zitamlipa kulingana na soko”

 

 

Akifafanua juu ya bidhaa maalumu amesema kuwa NBC inatoa fursa ya uwakala ambapo mstaafu akichangamkia ni moja ya biashara itakayompatia kipato. Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa sekta ya kilimo benki ya NBC inahuduma ya akaunti maalumu ya wakulima iitwayo NBC Shambani inayolenga kuwahudumia wakulima wakubwa, wa kati na wadogo.

 

 

“Tupo karibu na wateja wetu na tunaamini kuna wastaafu watakaojikita na kilimo hivyo tunawakaribisha” alisema. Akizungumza pia kwenye semina kama hiyo Mkoani Mtwara, Meneja wa benki hiyo tawi la Mtwara Emmanuel Mseti aliwaasa wastaafu hao watarajiwa kuhakikisha wanawashirikisha wataalamu wa fedha pindi wanapofikiria kuhusu mawazo ya biashara, uwekezaji na matumizi sahihi ya mikopo yao ili kujihakikishia ufanisi wa matumizi ya mafao yao.

 

 

“Ndio maana benki ya NBC tumekuwa na utaratibu mzuri wa kuwapatia mafunzo wateja wetu kupitia mipango mbalimbali ukiwemo mpango wa Klabu za biashara na utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kufanya biashara wateja wetu kabla hatujawajakopesha,’’ alisema.

 

 

Wito kama huo pia ulitolewa Zanzibar na Mkuu wa bidhaa na Mauzo wa Benki hiyo, Abel Kaseko ambapo aliwasihi wastaafu hao watarajiwa Zanzibar, kuhakikisha wanahifadhi pesa zao kwenye taasisi rasmi za kifedha ili kuepuka matapeli.

 

 

“Zaidi pia tuhakikishe tunaanza uwekezaji mapema ili kujijengea uzoefu utakaotusaidia kujiandaa na maisha ya baadae. Ifahamike kwamba matumizi sahihi ya fedha hizi ndio utakaosaidia wengi wetu kuondokana na utegemezi baada ya kustaafu,’’ alisema.

 

 

Pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa nasaha hizo muhimu, washiriki wa mafunzo hayo kutoka katika taasisi mbalimbali walielezea namna walivyonufaika na mafunzo hayo huku wakikiri kwamba wengi wao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kushindwa kujiwekea akiba, matumizi yasiyo sahihi ya mafao baada ya kustaafu na kushindwa kubuni mawazo mazuri ya uwekezaji wa fedha hizo.

 

 

“Niwashukuru sana watu wa PSSSF kwa kuhusisha wataalamu mbalimbali kwenye semina hizi zikiwemo benki kama NBC kwa kuwa wametufumbua macho kwenye mambo mengi na kwa kweli kupitia elimu hiyo itatusaidia sana,’’ alisema Bw Ali Mselem Ali, mstaafu mtarajiwa kutoka Zanzibar.

 

 

Semina hiyo ilipambwa na uwepo wa viongozi waandamizi wa serikali katika mikoa hiyo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti na   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango  Zanzibar Bw Rashid Said Rashid.

Leave A Reply