BENKI ya NMB imetwaa tuzo maalum kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kama Benki bora ya Taarifa za Kifedha zilizokaguliwa na kutambuliwa kimataifa kwa mwaka 2018, ilyoshinda benki kadhaa nchini.
Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imetoa shukrani kwa wafanyakazi na kujivunia mfumo bora wa Uongozi na utendaji hasa kitengo cha fedha. “Tuzo hii imepatikana nyuma ya mfumo uliopo wa utawala bora na michakato ya udhibiti ambayo inakuza uwazi wa taarifa za kifedha, uwajibikaji, ueledi na kiwango cha juu cha uadilifu wa takwimu. Hongera kwa kila mtu, haswa timu ya kifedha kwa kuongoza maandalizi ya Taarifa ya Fedha ya Benki ya NMB.