The House of Favourite Newspapers

BENKI YA NMB YAWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA KIBAHA

Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha pongezi kwa kufanya biashara kwa uaminifu, mmoja wa wafanyabiashara kilichotolewa na Benki ya NMB kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha akimkabidhi cheti maalum cha pongezi kwa kufanya biashara kwa uaminifu, Bi. Salome Shayo kilichotolewa na Benki ya NMB kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana.
Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Baraka Ladislaus (katikati) akizungumza na wafanyabiashara kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha jana. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kibaha, Hosea Lyatou (wa kwanza kulia) wakifuatilia warsha hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB Idara ya Biashara Makao Makuu, Bw. Wogofya Mfalamagoha (kulia) akizungumza na wafanyabiashara hao(hawapo pichani).
Meneja Mahusiano Biashara wa Benki ya NMB, Kanda ya Mashariki, Bi. Prisca Lius (kushoto) akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabiashara (hawapo pichani) kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha. Kongamano hilo lililokuwa na kaulu mbiu ya ‘Habaki Mtu…tunasonga Mbele Paamoja’ liliandaliwa na Benki ya NMB.
Meneja wa Benki ya NMB Kibaha, Hosea Lyatou (kulia) akimpongeza mmoja wa wafanyabiashara (kushoto) mara baada ya kutunukiwa cheti maalum na Benki ya NMB kwa kufanya vizuri zaidi katika biashara yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa True Maisha Training Company, Erick Chrispin aakiwasilisha mada kwenye Kongamano la Wafanyabiashara lililoandaliwa na Benki ya NMB Wilayani Kibaha.
Mmoja wa washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha akiuliza swali jana mara baada ya kupata mafunzo namna ya kukuza biashara zao. Kongamano hilo lililokuwa na kaulu mbiu ya ‘Habaki Mtu…tunasonga Mbele Paamoja’ liliandaliwa na Benki ya NMB.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha wakiuliza maswali mara baada ya kupata mafunzo namna ya kukuza biashara zao. Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu ya ‘Habaki Mtu…Tunasonga Mbele Pamoja’ liliandaliwa na Benki ya NMB.
Meneja Mikopo NMB Kibaha, Alfred Matovelo akizungumza na wafanyabiashara katika kongamano hilo.
Sehemu ya washiriki katika Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB wilayani Kibaha wakifuatilia mada mbalimbali.

Comments are closed.