Benki Ya Taifa Ya Biashara (NBC) Yazindua Kampeni Mpya Ya “Shinda Mechi Zako Na NBC”
Dar es Salaam 3, Mei, 2023: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imezindua kampeni mpya inayojulikana kama “Shinda Mechi Zako na NBC”. Kampeni ya “Shinda Mechi Zako na NBC”, inalenga kuongeza thamani kwa wateja wa NBC na kukuza ukuaji wao wa kifedha na uchumi wa nchi. Kampeni ina lengo la kuwafikia wateja binafsi, waajiriwa, wamiliki wa biashara ndogo, mawakala, na wengine wanaotumia huduma za benki za kimtandao kupitia NBC.
Kwa kutambua changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wa kada mbali mbali, Benki ya NBC imepanga kuwasaidia kutatua changamoto hizo kupitia ushauri na huduma za kifedha ambazo ni suluhisho za changamoito hizo na mechi na hivyo kuja na jina “Shinda mechi zako na NBC”.
Kupitia kampeni hii NBC imetumia baadhi ya wachezaji nyota wa ligi kuu ya NBC. Kupitia kampeni hii, wateja wataweza kunufaika na gharama nafuu za miamala kama vile kuweka standing order bure kabisa, kulipia kwa kadi huduma za mtandaoni kwa punguzo la bei, na upatikanaji wa mikopo binafsi na ya biashara hadi milioni 150 ndani ya masaa 48. Aidha, wateja wanaweza kupata faida ya hadi asilimia 7% kwenye akaunti zao za NBC Malengo. Wateja pia wanaweza kupata mkopo wa kumalizia nyumba kwa gharama nafuu ili kukamilisha ndoto zao za ujenzi wa nyumba.
Kampeni ya “Shinda Mechi Zako na NBC” inalenga kuimarisha ustawi wa kifedha wa wateja wa NBC na kusaidia juhudi za serikali katika kutoa huduma za kifedha, kukuza uchumi wa watanzania. NBC inaamini kuwa kampeni hii itawapa wateja faida kubwa na kuboresha thamani na uzoefu wa benki yao.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kanpeni hiyo, Mkuu wa Bidhaa za NBC, Abel Kaseko alisema, “Tuna furaha kuzindua kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako na NBC’, ambayo ipo kwa ajili ya kuwapa nguvu wateja wetu na kuwasaidia kufikia malengo yao ya kifedha kwa kuongeza thamani na uzoefu wao wa benki. Kampeni hii itawapa wateja wetu huduma za KIbenki zenye gharama nafuu na rahisi, na pia kusaidia kukuza uchumi wao.”
Kwa upande wake Mkuu wa Masoko ya NBC, David Raymond, alisema, “Tuna furaha kuzindua kampeni ya ‘Shinda Mechi Zako na NBC’ kwani ni sehemu ya ahadi yetu ya kuendelea kutoa huduma nafuu na rahisi za kibenki zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu. Tunaamini kuwa huduma hizi zitawasaidia wateja wetu kutimiza malengo yao ya kiuchumi na kijamii na pia kuchangia katika ukuaji wa uchumi binafsi na wa taifa kwa ujumla.”
Pamoja na malengo mengine, Kampeni inalenga kukuza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuhamasisha zaidi watanzania kutumia huduma za benki. Pia ni sehemu ya ahadi kubwa ya NBC ya kusaidia juhudi za serikali ya Tanzania katika kukuza uchumi jumuishi.