The House of Favourite Newspapers

Benki ya UBA Yahitimisha Wiki ya Huduma Kwa Wateja Kwa Kuwashukuru Na Kuwapongeza Wateja Na Watoa Huduma Wake

0
Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Bank’s, Mr. Gbenga Makinde (kulia ) akimpa kinywaji mmoja wa wateja wa muda mrefu wa benki hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Amour Mohammed katika kusherehekea wiki ya Huduma kwa Wateja (kushoto) ni Afisa wa Kitengo cha Wateja Wakubwa, Dora Kyungu.

Dar es Salaam, 6 Oktoba 2023: Benki ya UBA imehitimisha ‘Wiki Ya Huduma Kwa Wateja’ kwa kuwapongeza wateja wake pamoja na watoa huduma wa benki kwenye hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo yaliyopo Barabara ya Nyerere jijini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Mr Gbenga Makinde amesema;

“Nipende kutumia nafasi hii ya Wiki ya Huduma ya Huduma kwa Wateja kuwapongeza na kuwashukuru wateja wetu wote pamoja na wafanyakazi wetu ambao wametufikisha kwenye mafanikio haya makubwa tuliyofikia.

“Wote hao kwa pamoja kwa kujitolea kwao kuwa na benki ya UBA ndiyo mafanikio haya tunayoyona na kuyasherehekea leo hii, bila nguvu ya umoja na uaminifu wao kwa benki hii leo hii tusingefikia manikio haya tunayosherehekea leo hii katika Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Kwa Upande wake Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki hiyo, Flavia Kiyanga ameungana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, kwa kuwapongeza na kuwashukuru wateja na watoa huduma wa benki hiyo na kuongeza kwa kusema;

“Pamoja na shukrani hizo kwa wateja na watoa huduma wetu nipende pia kusema sasa hivi benki yetu imejitanua zaidi na sasa hivi tupo karibia mikoa yote kwasababu ya mawakala wa kibenki.

“Tuna mawakala zaidi ya mia saba Tanzania nzima kwahiyo hata wakazi wa vijijini nao wanaweza kupata huduma zetu bila wasiwasi wowote na wasiotumia huduma zetu tunaomba waanze kufanya hivyo sasa.

“Pamoja na mawakala hao pia tumefungua matawi kwa wingi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Arusha, Mwanza na mikoa mingineyo.

“Kwahiyo huduma zetu zinakua hivyo kupitia wiki hii ya Huduma kwa Wateja tunawaomba wateja wetu wazidi kutuamini na tunawaahidi kutoa huduma bora siku zote”. Alimaliza kusema Flavia Kiyanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Bank’s, Mr Gbenga Makinde (katikati), Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa benki hiyo, Flavia Kiyanga (kulia) wakikata keki pamoja na mteja wa muda mrefu katika benki hiyo, Amour Mohammed (kushoto) katika hafla ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Akizungumza kwa niaba ya wateja wa benki hiyo, Amour Mohammed amesema yeye ni mteja wa benki kwa zaidi ya miaka kumi sasa na amekuwa akifurahia huduma za benki hiyo ambazo hazina usumbufu ambao amekuwa akikutana nao sehemu zingine.

Amour amewashauri watumiaji wengine wa huduma za kibenki kutumia huduma za benki zilizosambaa nchini nzima.

Leave A Reply