The House of Favourite Newspapers

Manula Aleta Tabasamu Simba kipa Ayoub Lakred Atajwa

0

WAKATI mashabiki wa Simba baadhi wakiwa hawana imani na kipa Ayoub Lakred kutokana na kuruhusu mabao katika mechi mbili za kimataifa, tabasamu limeanza kuonekana baada ya Aishi Manula kuanza mazoezi ya uwanjani.

Manula ambaye ni kipa namba moja wa Simba, amerejea kwenye uwanja cha mazoezi mara baada ya kuwa nje muda mrefu akiuguza majeraha ya mguu.

Manula ameanza rasmi mazoezi na magolikipa wenzake ndani ya klabu hiyo tofauti na awali alipokuwa akifanya binafsi kwa takribani wiki tatu.

Kwa mujibu wa duru za habari kutoka kwenye uongozi wa Simba, zinasema kuwa Manula kwa sasa yupo tayari kwa ajili ya kukaa kwenye milingoti mitatu ya Simba.

Kocha wa Makipa wa Simba, Dani Cadena, alisema: “Haya ni mazoezi ya nne baada ya kuumia. Nina furaha kwa mabadiliko yanayoonekana kidogokidogo.”

Leave A Reply