The House of Favourite Newspapers

Bernabeu Na Emirates Kuwaka Moto Leo Ligi Ya Mabingwa Ulaya

0

Viwanja viwili vitawaka moto leo kwenye ligi ya mabingwa ulaya hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, Ambapo vilabu vya Real Madrid na Arsenal vitakua nyumbani kuwakaribisha Man City na Bayern Munich.

Santiago Bernabeu ambapo ndio uwanja wa nyumbani wa klabu ya Real Madrid ndipo moto utakapowaka leo ambapo watawakaribisha mabingwa watetezi wa michuano hiyo klabu ya Man City, Huku kule Emirates pia kukipigwa kipute kikali ambapo Arsenal watakua nyumbani kuwakaribisha klabu ya Bayern Munich.

Real Madrid watakwenda kumenyana na klabu ya Manchester City wakiwa kwenye fomu nzuri kwelikweli, Kwani mpaka sasa wanaongoza ligi kuu nchini Hispania huku Man City nao wakiwa sio haba licha ya kuandamwa na majeraha ya hapa na pale.

Real Madrid wataingia kwenye mchezo huu kwanza kutafuta ushindi utakaowaeka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali, Lakini pia kulipa kisasi kwa kilichowakuta mbele ya Man City msimu ulimalizika ambapo walitupwa nje ya michuano hiyo kwa kipigi kikubwa cha mabao manne kwa bila.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Mchezo mwingine utakua baina ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya soka ya Arsenal ambapo watakipiga dhidi ya klabu ya Bayern Munich katika dimba lao la Emirates mchezo mwingine ambao unatarajiwa kua mkali na wenye ushindani mkubwa.

Ikumbukwe pia mchezo hautakua wakawaida kwani Arsenal nao watahitaji kufuta uteja wa muda mrefu ambao wamekua nao mbele ya klabu ya Fc Bayern Munich, Hivo mchezo wa leo pia ni wa kulipa kisasi kwa klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa jiji la London.

Vilabu hivi vinakutana kipindi ambacho Bayern Munich wanaonekana hawako kwenye ubora mkubwa huku Arsenal wao wakiwa kwenye fomu ya maisha yao, Jambo ambalo linafanya mashabiki wengi wa soka kuamini unaweza kua wakati sahihi wa Arsenal kulipa kisasi cha mateso ya muda mrefu ambayo wamekua wakipitia mbele ya Bayern Munich.

Michezo yote ya leo inapatikana pale Meridianbet na imepewa ODDS KUBWA ambazo zinaweza kukufanya ukaibuka na mkwanja wa kutosha, cha kufanya ni wewe kutengeneza mkeka wako kupitia michezo hii ya kukata na shoka uweze kupiga mkwanja.

 

Leave A Reply