The House of Favourite Newspapers

Betika Latinga Ubungo River Side, Makoka

MAPEMA leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers imetembelea maeneo ya Ubungo River Side, Makoka na maeneo ya Kariakoo Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kulitangaza zaidi Gazeti la Betika.

Betika ambalo hutolewa bure kwa wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kuwa gumzo kila kona.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Comments are closed.