The House of Favourite Newspapers

Bi Sonia wa Bongo Movies Afariki Dunia, Mastaa Mbalimbali wa Filamu Wamlilia

0
Farida Sabu maarufu kama Bi Sonia amefariki dunia

FARIDA Sabu almaarufu Bi Sonia; ni mkongwe mwingine wa Bongo Movies ambaye amefariki dunia leo, Julai 21, 2022 ikiwa ni siku chache tangu kifo cha mkongwe mwingine wa tasnia hiyo, Bi Hindu.

 

Habari zilizothibitishwa na baadhi ya waigizaji wenzake zinasema kuwa, Bi Sonia amefikwa na umauti visiwani Zanzibar ambapo taratibu za mazishi zinafanyika.

 

Baadhi ya waigizaji waliotoa pole ni pamoja na Monalisa ambaye amepsti picha ya Bi Sonia na kuandika; “Omg!! Pumzika kwa amani mama yetu Farida Sabu…”

 

Kisha Swebe Santana; “Innalillah wainna ilayhi raajiuun…Mama Farida Sabu umeumaliza mwendo… Poleni sana Familia…Wasanii…”

 

Bi Sonia alifanya vizuri mno enzi za Kaole Sanaa Group katika Tamthiliya ya Tufani kisha tamthiliya za sasa za Ndoano na Juakali. R.I.P BI SONIA!
Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply