The House of Favourite Newspapers

Bigirimana atumika utapeli Dar

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Mnyarwanda, Issa Bigirimana ‘Walcott’ amekiona cha moto baada ya ‘wahuni’ kufanya utapeli kwa kutumia akaunti yake.

 

Mnyarwanda huyo ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, wengine baadhi ni Patrick Sibomana, Maybin Kalengo, Farouk Shikaolo na Sadney Urikhob.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Sibomana alisema kuwa watu wasiojulikana wametengeneza akaunti ‘fake’ ya Instagram wanaoitumia vibaya kuwatapeli baadhi ya mashabiki wa Yanga.

Sibomana alisema kuwa utapeli huo ulianza mara baada ya kusajiliwa na kutangazwa mchezaji wa Yanga huku akiwatahadharisha mashabiki wa Yanga kuwa makini na matapeli hao wanaotaka kujipatia fedha kwa kutumia jina lake.

 

Aliongeza kuwa, matapeli hao wanatumia akaunti hizo alizozitaja nne kwa ajili ya udanganyifu kujipatia fedha kwa kuwaomba mashabiki wa Yanga.

 

“Labda niwatajie akaunti yangu ninayoitumia kwenye akaunti zangu za Instagram na Facebook kuwa natumia Issa Walcott na siyo Issa Bigirimana, ni vema wakalifahamu hilo katika kuepuka kutapeliwa na vibaka.

 

“Zipo akaunti nne ‘fake’ zilizotengenezwa na wezi hao ambazo siyo zangu, wanazitengeneza kwa nia mbaya ya kutaka kuwaibia mashabiki wa Yanga kwa kuwaomba fedha.

 

“Niwaombe hao wezi kuachana na hizo akaunti, sitaki kuona hili likiendelea la wizi wa fedha na mashabiki wa Yanga hiyo nyingine ndiyo akaunti yangu,” alisema

Comments are closed.