The House of Favourite Newspapers

Bilionea Gertler, Swahiba wa Kabila Aliyewekewa Vikwazo na Marekani

0

Utawala wa Biden hivi karibuni umemuwekea tena vikwazo mfanyabiashara wa Israeli Dan Gertler juu ya madai ya ufisadi mkubwa kwenye biashara ya madini katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

 

Mwanahabari Franz Wild ameangazia kuongezeka kwa umaarufu wake na ushirikiano wake na aliyekuwa Rais Joseph Kabila kipindi ambacho pia aliteuliwa kama mwanadiplomasia wa Congo.

 

 

Mara ya kwanza Marekani inamuwekea vikwazo katika biashara ya madini mwaka 2017, aliajiri wakili wa Rais Donald Trump ili aondolewe vikwazo hivyo.

 

 

Vikwazo hivyo alikuwa amewekewa kwa madai ya uhusiano wake wa kifisadi na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila, aliyemsaidia katika utajiri wake kutokana na makubaliano ya madini ya shaba na kobalti nchini humo jambo ambalo wote wawili wamelikanusha.

 

 

Msemaji wa Bwana Gertler amesema kuwa madai hayo “ni ya kiuonevu dhidi yake” na kuongeza kuwa “hakuna ushahidi hata chembe unaothibitisha madai hayo”.

 

Aliondolewa vikwazo na Trump

Kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili, Bwana Gertler, ambaye ana umri wa miaka 47, alikuwa mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini humo.

 

 

Alikuwa na ushawishi mkubwa katika ufanyaji maamuzi wa ni kampuni gani zingeruhusiwa kuendeleza shughuli za madini katika vyanzo vya madini ya shaba, kobalti, bati, dhahabu na almasi.

 

 

Kuna kipindi, Bwana Gertler pia alikuwa mjumbe muhimu katika masuala ya kidiplomasia kwa Bwana Kabila. Na kumuajiri wakili wa Bwana Trump katika kesi iliyokuwa inamkabili kulidhihirisha mafanikio yake.

 

 

Siku za mwisho, utawala wa Bwana Trump ulimruhusu Bwana Gertler leseni katika vikwazo alivyokuwa amewekewa na kumruhusu kufikia pesa zake zilizokuwa zimepigwa tanji pamoja na mfumo mzima wa benki kimataifa kwa mwaka mmoja.

 

 

Mnamo mwezi Machi, mali yake ilirudishwa kwa kasi ya ajabu. Marekani itaendelea kuwajibisha wanaodaiwa kuendeleza ufisadi kwa kutumia kila njia tunayoweza” alisema, Ned Price, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje.

 

 

Vikwazo vilikuwa lazima “kukabiliana na ufisadi na kuendeleza udhibiti katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo,” Bwana Price amesema.

 

 

Katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo, Bwana Gertler alikuwa kama wakala kati ya nchi hiyo na makampuni ya kimataifa kwa niaba ya Bwana Kabila, kulingana na tangazo la vikwazo lililowekwa na Marekani.

 

 

Na kwasababu Rais Felix Tshisekedi amekuwa madarakani tangu mwaka 2019, anaendelea kupambana na wadhibiti wa Bwana Kabila katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Marekani inataka Bwana Gertler pia naye adhibitiwe.

 

Bilionea Gertler, chanzo cha Kabila kuungwa mkono na Rais Bush

Aliyekuwa kijana wa mpenda soka aliyekuwa na mafanikio makubwa katika familia ya wafanyabiashara mkubwa Tel Aviv, Bwana Gertler aliwasili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1997, muda mfupi baada ya baba yake Bwana Kabila, Laurent-Desirée, kuingia madarakani.

 

 

Mwaka 2000, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyohatarisha kumaliza utawala wa Bwana Kabila muda mfupi baada ya kuanza, Bwana Gertler aliahidi mamilioni ya madola, kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa, ufikiaji wa silaha – vitu viwili muhimu ambavyo vingemsaidia kiongozi mpya kuingia madarakani.

 

 

Na matokeo yake, akawa ni muuzaji pekee wa madini ya almasi nje ya nchi. Bwana Gertler aliaminiwa zaidi na Bwana Kabila, ambaye alichukua hatamu kama rais baada ya mauaji ya baba yake mwaka 2001.

 

 

Akiwa vitani na Marekani na Rwanda, kiongozi mchanga alimtuma Bwana Gertler Washington kuomba kuungwa mkono na Rais George W Bush.

 

 

Baada ya majadiliano marefu na Bwana Gertler, utawala wa Bush ulikubaliana kumuunga mkono Bwana Kabila, na kusaidia kufikiwa kwa makubaliano ya amani kati ya pande zilizokuwa pinzani na utawala wa Bwana Kabila.

 

 

Bwana Gertler pia alikuwa balozi wa heshima nchini Israel na pasipoti ya kidiplomasia. ‘Alitoa hongo ya dola milioni 100 kama ufisadi’

 

 

Kampuni zilizodhibitiwa na Bwana Gertler zilianza kupata leseni za utekelezaji wa biashara ya madini kote nchini humo. Mara nyingi alisaidia kampuni za kimataifa kama vile ya Glencore ya Uswizi na ya Och-Ziff ya Marekani ambazo zilijipatia faida kubwa.

 

 

DR Congo ina raslimali nyingi za madini ikiwemo zaidi ya asilimia 60 ya madini ya kobalti duniani. Kabla ya kampuni ya Och-Ziff kuwekeza kwa Bwana Gertler, ikaagiza kupitiwa tena kwa namna anavyofanya kazi.

 

 

Amekuwa “tayari kutumia ushawishi wake wa kisiasa na Bwana [Kabila]… na kutumia nafasi yake katika upatikanaji wa kandarasi, kutatua migogoro na kutatiza washindani,”

 

 

Majina ya Bwana Gertler na Bwana Kabila yalikuwa yakitajwa katika Wizara ya sheria lakini walitambuliwa kwa nyakati tofauti.

 

 

Katika makubaliano yake na Wizara ya Sheria, kampuni ya Och-Ziff ilikubali kuwa Bwana Gertler alikuwa amelipa dola milioni 100 kama rushwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo madai ambayo Bwana Gertler ameyakanusha.

 

 

Kadri muda ulivyosonga, kuliendelea kuwa na maswali kwasababu ya makubaliano yaliyofikiwa na Bwana Gertler na alialika wanahabari kuangazia miradi yake jinsi ilivyokuwa inanufaisha DR Congo, hata kama madai dhidi ya ufisadi hayakuelezwa.

 

 

Maisha chini ya utawala mpya

Kampuni ya Och-Ziff ilizidisha madai dhidi ya kampuni hiyo. Ripoti iliyoanzishwa na kampuni ya Africa Progress Panel ilisema kuwa DR Congo ilikuwa imepoteza karibu dola bilioni 1.36 katika makubaliano na Bwana Gertler kati ya mwaka 2010 na 2012 pekee. Na Marekani ikaweka vikwazo.

 

 

Lakini licha ya hayo yote, ndege ya kibinafsi ya Bwana Gertler iliendelea na safari zake za kila mara hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

 

 

Vikwazo vilivyosimamishwa kwa muda dhidi ya Bwana Gertler havikudumu muda mrefu na kuna uwezekano mkubwa vilimuwezesha kutatua matatizo yake ya kifedha.

 

 

Changamoto kwake itakuwa kuendeleza ushawishi wake katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako hadi sasa hivi hajaguswa.

 

 

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Tshisekedi miaka miwili iliyopita, amekuwa akifuatilia waliokuwa na nguvu katika utawala wake.

 

 

Katika wiki za hivi karibuni, Bwana Tshisekedi ameingiza madarakani wale ambao ni waaminifu kwake kuongoza serikali na bunge.

 

 

Kwa raia wengi wa Congo, Bwana Gertler anaonesha vile ufisadi ulivyokuwa katika utawala wa Bwana Kabila. Ikiwa Bwana Gertler ataendelea kuwa na ushawishi chini ya rais wa sasa ndio changamoto kubwa.

 

Leave A Reply