The House of Favourite Newspapers

Billnass: Sijarudiana na Nandy!

0

BAADA ya msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ hivi karibuni kudaiwa kurudiana na mpenzi wake wa zamani ‘Billnass’ jamaa huyo ameibuka na kusema kwamba hana uhusiano wowote wa kimapenzi na mrembo huyo.

Akizungumza na gazeti Mikito Nusunusu, Billnass amesema kwamba hajawahi kurudiana na Nandy kama ambavyo watu wengi wanasema, bali wao ni washikaji tu kama walivyo watu wengine.

“Mimi ndio nakwambia wewe leo kuwa Nandy sio mpenzi wangu na wala mimi na yeye hatujawahi kurudiana, au umewahi kusikia mimi na Nandy tunasema popote kuwa tumerudiana? Kwa hiyo watu wanaongea tu mambo wasiyo na uhakika nayo,” alisema Billnass.

 

 

STORI: MEMORISE RICHARD

Leave A Reply