The House of Favourite Newspapers

Bingwa mashindano ya Ufukweni Ajishindia Milioni Moja

TIMU mbalimbali zimejitokeza kushiriki mashindano ya mpira wa miguu yan ufukweni katika kusherehekea siku ya Usafi wa Bahari Duniani pamoja na kuuunga mkono Kampeni ya Serikari ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya Plastiki.

Katika kuadhimisha siku hiyo Makampuni mbalimbali jijini Dar es Salaam yaunga usafi ufukwe wa Coco Beach katika kuadhimisha mwezi wa usafi Baharini ambapo huadhimishwa Juni 8 kila mwaka pamoja na kuunga mkono Kampeni ya Serikali ya matumizi ya mifuko ya Plastiki.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mwakilishi wa waratibu wa shughuli hiyo kutoka Kampuni ya Verge of Africa, Hafsa Mambosasa alisema wao kwa kushirikiana na makampuni rafiki wameungana kufanya shughuli hii ya kijamii ikiwa ni sehema ya kuihamasisha jamii kuwa swala la kutunza mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu.

Mratibu Hafsa aliyataja makampuni yaliyojitokeza kuwa ni Kampuni ya vinywaji ya Pepsi, Red Bull, Hoteli ya Slipway, G1 Security Limited, AfyaPal(Muhimbili) na Nipe Fagio.

Comments are closed.