The House of Favourite Newspapers

Black Panther Kuunguruma Novemba 2022

0

FILAMU iliyopendwa na wengi duniani kwa namna wahusika wake walivyo wa kipekee na waliobeba asili na tamaduni za Kiafrika, Black Panther itaachiwa tena rasmi Novemba 2022, hii inakuja kufuatia kampuni ya Disney inayoshirikiana na kampuni ya Marvel kuchelewesha utengenezaji wa filamu hiyo.

 

Black Panther kwa mara ya kwanza ilioneshwa rasmi, Januari 29, mwaka 2018 huku ikiwa na mastaa kibao wenye asili ya Afrika na Marekani;  Chadwick Boseman, Lupita Nyongo, Michael B. Jordan, Martin Freeman na wengineo.

 

Sambamba na filamu hiyo, pia kampuni ya Disney imeweka wazi kusogeza mbele siku ya kuachia filamu zingine kama; The Marvel ambayo itatoka Februari 2023 huku Ant-Man ikitarajiwa pia kutoka Julai 2023.

Cc; @bakarimahundu

Leave A Reply