The House of Favourite Newspapers

Blatter, Platini wafungiwa miaka 8 kutojihusisha na soka

0

Michel-PlatiniSepp-Blatte-001Platini (kushoto) akiwa na Blatter

Zurich, Uswisi
Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Sepp Blatter na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Fifa na Rais wa Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), Michel Platini, wamekutwa na hatia katika sakata la rushwa na matumizi mabaya ya ofisi yaliyokuwa yakiwakabili na kila mmoja amefungiwa miaka 8 kutojihusisha na masuala yoyote yanayohusu mchezo wa soka.

PlatiniBlatter (kushoto) akiwa na Platini

Hukumu hiyo imetolewa na kamati ya maadili ya Fifa leo Jumatatu na inatarajiwa kuanza mara moja, huku wawili hao wakipewa muda wa kukata rufaa kama hawajaridhishwa na hukumu hiyo.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, mbali na makosa mengine, Blatter aliidhinisha kiwango kikubwa cha dola za Kimarekani milioni 2 kwa Platini, mazingira ambayo baadaye imebainika kwamba yalijaa rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.
Blatter tayari alikuwa amesimamishwa wadhifa wake kama rais wa shirikisho hilo ili kupisha uchunguzi kwa tuhuma zilizokuwa zinamkabili na zilikuwepo taarifa kwamba Platini huenda angerithi nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa Fifa unaotarajiwa kufanyika Februari 26, mwaka huu lakini baada ya hukumu kutoka, ndoto hiyo imezimika ghafla.
Mbali na kufungiwa, Blatter amepigwa faini ya dola za Kimarekani 50,250 na Platini amepigwa faini ya dola za Kimarekani 80,400.

Leave A Reply