The House of Favourite Newspapers

Bobi Wine Akamatawa Akifanya Kampeni za Mwisho Uganda

0

POLISI wa Kasangati, Wilaya ya Wakiso nchini Uganda leo wamemkamata mgombea binafsi wa kiti cha ubunge cha Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi Sentamu ambaye ni maarufu kama Bobi Wine.

Wine alikamatawa leo wakati akijaribu kuwahutubia wafuasi wake huko Kasangati ambapo polisi walimpeleka katika kituo cha Divisheni ya Kira baada ya wafuasi wake kufanya fujo wakitaka aachiliwe ambapo walivamia kituo hicho cha polisi.

Pamoja na yote hayo, haijajulikana iwapo mtu huyo atafunguliwa mashitaka. Polisi walisema Kyagulanyi alikuwa ameonywa mapema asitumia eneo hilo kwani Rais Yoweri Museven alikuwa karibu na eneo hilo kiasi cha kilomita moja kutoka hapo.

Rais Museveni yuko jimboni humo kumpigia kampeni mgombea wa chama cha NRM, Sitenda Sabulu.

 

Nishushe Dar Live: Roma, Stamina Waweka Historia Dar Live (Pichaz + Videos)

Leave A Reply