The House of Favourite Newspapers

Bocco akubali mziki wa Yanga SC

0

NAHODHA na mshambuliaji wa Simba, John Bocco amekiri kuzidiwa kiwango dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga kilichosababisha wafungwe bao 1-0.

 

Yanga imewafunga Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

Katika mchezo huo uliojaa na upinzani mkubwa, bao la ushindi la Yanga lilifungwa na Fiston Mayele kwa shuti kali dakika ya 11.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Bocco alisema kuwa pongezi kubwa ziende kwa Yanga ambao walicheza soka safi ambalo liliwapa matokeo mazuri.

 

Bocco alisema kuwa katika mchezo huo timu yao ilizidiwa katika safu ya kiungo na hiyo imetokana na uimara wa viungo wa wapinzao wao.

 

Aliongeza kuwa licha ya kufungwa dhidi Yanga, lakini wanajutia baadhi ya nafasi walizozitengeneza kama wangezitumia vizuri, basi matokeo yasingemaliza hivyo.

 

“Lipo wazi wapinzani wenzetu walikuwa bora katika mchezo huu, hiyo ndiyo sababu ya sisi Simba kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

 

“Walistahili ushindi kutokana na kucheza kwa tahadhari kwa kucheza kwa kushambulia na kulinda lango lao ndani ya wakati mmoja.

 

“Hivyo makocha wetu wameona upungufu wa timu yetu ambao watakwenda kuufanyia kazi ili tupate matokeo mazuri katika michezo ya Ligi Kuu Bara,” alisema Bocco.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply