The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu Arudisha Majeshi kwa Prezzo

0

PENZI ni kikohozi hivyo kulificha huwezi! Ni msemo wa Wahenga lakini sasa unafanya kazi kwani sio siri tena kwamba, msanii wa Bongo Fleva, Amber Lulu amerejesha majeshi rasmi kwa aliyekuwa mwandani wake, Rapa Prezzo wa nchini Kenya.

 

Amber lulu na Prezzo waliwahi kuwa wapenzi kabla ya Amber Lulu kunyakuliwa na jamaa ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kike ambaye naye amemwagana naye.

 

Kupitia kurasa zake za kijamii na Insta Story yake, Amber Lulu ameweka screenshot akiongea na Prezzo kisha akasindikiza na maandishi yaliyosomeka; “True love never die (mapenzi ya kweli hayafi!”

 

Wataalam wa mambo wameibuka na kusema kwamba, hiyo ni ishara tosha kwamba wawili hao wamerudiana kwani walipendana mno kipindi hicho.

STORI; IJUMAA WIKIENDA, DAR

Leave A Reply