The House of Favourite Newspapers

Bodaboda apigwa risasi

0

IMG_0373

Yusuf Ramadhan.

Haruni Sanchawa

KIFO njenje! Kijana Yusuf Ramadhan (26), mkazi wa Chamazi jijini Dar, amenusurika kuuawa baada ya kupigwa risasi shavuni na mtu anayesadikika kuwa ni jambazi aliyekuwa amelenga kumpora pikipiki yake aina ya boksa.

Akisimulia mkasa huo akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar, kijana huyo alisema kwamba, ilikuwa hivi karibuni ambapo alikodiwa na abiria kutoka maeneo ya Mbande hadi Chamazi.

Alisema kuwa alipofika sehemu huko Chamazi, abiria huyo alimwambia amefika hivyo amshushe, akiwa bado anasubiria kulipwa ndipo akatokea mtu porini na kumpiga risasi ya shavu la kulia.

IMG_0374“Lengo la yule jamaa lilikuwa ni kupora pikipiki yangu, kelele zangu na abiria ndizo zilizonifanya niwe hai leo ingawa risasi bado haijatolewa shavuni, madaktari wanaendelea kunifanyia vipimo zaidi ili waweze kuiondoa mwilini mwangu,” alisema Ramadhani akisikilizia maumivu makali.

Kijana Ramadhani anaishi na risasi hiyo kwenye shavu la kulia akiwa amelazwa kwenye wodi namba 23 katika Jengo la Sewa Haji Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Majeruhi huyo anaomba msaada kwani hali yake kiuchumi baada ya kupatwa na masaibu hayo imekuwa mbaya na ndugu zake hawana uwezo.

“Hapa nilipo nipo katika wakati mgumu kifedha na kuna mahitaji mengi yanahitajika hivyo nawaomba Watanzania wenzangu wanisaidie ili niweze kujikimu,” alisema kijana huyo.

Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana naye kwa kutumia simu 0717 099635.

Leave A Reply