The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Usajili Majenzi Yaasa Wanafunzi kupenda Masomo ya Sayansi

0

Afisa Usaji wa AQRB, Bw. Teobad Gwimile akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee kuhamasisha fani za Ubunifu na Ukadiriaji Majenzi.

BODI ya Usajili wa Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) leo imefanya ziara katika baadhi ya shule za Sekondari jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi na hatimaye baadae kujiunga na fani ya Ubunifu na Ukadiriaji Majenzi ambayo imekuwa na wataalam wachache ukilinganisha na mahitaji ya wataalam hao.

 

Shule zilizofanikiwa kupata fursa hiyo ya uhamasishaji wanafunzi ili baadae watakaofanikiwa kujiunga na fani hiyo, ni pamoja na Shule za Sekondari Kinondoni Muslim na Shule ya Sekondari ya Jitegemee.

Afisa Mafunzo Mkuu, Daniel Matondo (Mbunifu Majengo) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kinondoni Muslim ya jijini Dar es Salaam kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na kujiunga na fani ya Ubunifu na Ukadiriaji Majenzi.

Akizungumza katika ziara hiyo, ya  wataalam kutoka AQRB, Afisa Mafunzo Mkuu, Daniel Matondo (Mbunifu Majengo) aliwataka wanafunzi kupenda masomo ya sayansi tangu awali jambo ambalo litawasaidia kujiunga na fani hiyo na kuongeza wataalam katika fani hiyo ili waje kulisaidia taifa.

Afisa Mafunzo Mkuu, Daniel Matondo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee ya jijini Dar es Salaam kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na kujiunga na fani ya Ubunifu na Ukadiriaji Majenzi.

Alisema mahitaji ya wataalamu wa ubunifu na Wakadiriaji Majenzi kwa sasa nchini Tanzania ni makubwa ukilinganisha na wataalam waliopo na ndio maana wamekuwa wakifanya ziara shuleni kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi ambayo ni msaada mkubwa kwa wataalam wa fani hizo hapo baadaye. “..Wewe mwanafunzi leo uwe kidato cha kwanza, chapili, cha tatu, cha nne, cha tano au cha sita unaweza kuanza kujiandaa baada ya kupata elimu hii ya uelewa juu ya Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi, kwamba usome masomo gani na kuyazingatia kama utapenda kujiunga na fani hiyo,” Bw. Matondo.

Picha ya kumbukumbu ya baadhi ya wanafunzi na wageni wao mara baada ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake, Afisa Usaji wa AQRB, Bw. Teobad Gwimile akizungumza na wanafunzi hao alisema fani hiyo ni muhimu katika taifa na inalipa hivyo wanafunzi wana kila sababu ya kuanza kuipenda tangu wakiwa katika atua za awali za masomo yao. Alisema wataalam hao hulisaidia taifa kuwa na majengo ya kisasa yenye mvuto na yaliobuniwa kulingana na maitaji ya eneo husika pamoja na hali ya hewa. “AQRB tutafurahi hapo baadaye tukija kusikia miongoni mwa wataalam hao ni nyinyi ambao umebahatika kupata elimu hii,” aliongeza Bw. Gwimile.

Leave A Reply