The House of Favourite Newspapers

‘Bodyline’ Yazindua Mashindano ya Ujenzi wa Mwili, Afya Dar

0
Kutoka kushoto ni Mwendesha Mafunzo, Haroub Mahamod; Mkurugenzi wa Bodyline Health and Fitness Centre, Abbas Jaffer na Kiongozi wa Tanzania Body Builiding Fereration (TBBF), Francis Mapugilo.

KITUO  cha Bodlyine Health and Fitness cha jijini Dar es Salaam kikishirikiana na Shirikisho la Mazoezi ya Kujenga Mwili (Tanzania Body Building Federation – TBBF) limezindua mashindano yajulikanayo kama Mission FitPossible kwenye kituo cha MayFair Plaza jijini kwa ajili ya kuwakutanisha wapenzi wa kujenga afya zao ambapo patakuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi.

Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi wa kituo hicho, Abbas Jaffer Ali, alisema pamoja na kuwakutanisha wapenzi wa kujenga afya zao ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa za kufanya mazoezi bure, lengo jingine kuu la zoezi hilo ni kukipa kizazi kijacho nchini, wanariadha watakaoshiriki michezo ya Olimpiki, washiriki wa mashindano ya kujenga mwili  na kutayarisha wanamichezo wengine mbalimbali.

.Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Mashindano hayo yatajumuisha kukimbia kutoka kituo cha Bodyline kupitia MayFair Plaza na Airtel Morocco kisha kurejea tena MayFair Plaza.

Kutakuwepo pia mafunzo ya maalum ya kujenga mwili yanayojulikana kama Aerobics, Spinners na SwimFit ambayo yatajumuisha pia uogeleaji.

Baadhi ya washiriki wa kutunisha misuli.

Vilevile, moja ya vilele vya tukio hilo ambalo kauli-mbiu yake ni ‘MICHEZO KA AJILI YA WOTE’ na watu wote wakikaribishwa kushiriki,  ni mashindano ya kumtafuta ‘Mr Bodyline’.

Kwa taarifa kamili tembelea www.globaltvtz.com

Na Denis Mtima/GPL

Leave A Reply