The House of Favourite Newspapers

Bohari ya Dawa Yanunua Mashine 140 za Kusafisha Damu kwa Wagonjwa wa Figo

0
Etty Kusiluka, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa MSD

 

Bohari ya Dawa nchini (MSD), imenunua mashine 140 kwa ajili ya kusafisha damu kwenye figo (dialysis) ambapo mashine tano tayari zishafungwa katika vituo vya hospitali mbalimbali.

Mashine hizo zimefungwa kwenye hospitali za Mwananyamala, Sekoutoure, Ilala na Tumbi huku nyingine zikiwa zinasubiri miundombinu ikamilike ili mashine hizo zifungwe na watu waanze kupata huduma ipasavyo na kwa bei nafuu tofauti na ilivyokuwa awali.

Meneja Udhibiti wa Bohari ya Dawa, Mwanashehe Juma amesema kuwa baada ya muda mfupi wagonjwa wa figo hawatapata shida ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Mwanashehe ameyasema hayo kwenye kikao kazi cha kwanza kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Bohari ya Dawa-MSD, kinachofanyika Jijini Dodoma.

Imeandikwa na Imelda Mtema

Leave A Reply