Bolt Yafurahishwa na LATRA Mwongozo Mpya wa Bei za Usafiri
Dar es Salaam 08 Januari 2023. Kampuni ya Bolt inafuraha kukujulisha kuwa LATRA imetoa notisi ya gazeti la serikali namba 7284, la tarehe 30 Disemba 2022 kuhusu mwongozo mpya wa bei za usafiri.
LATRA na wadau wengine wakuu katika tasnia hii wamekuwa na mikutano kadhaa, kufuatia kutolewa kwa Agizo la LATRA Na.01/2022, Machi 2022 ambapo LATRA iliweka ukomo wa kamisheniya 15%.
Bolt ilikubali kutii agizo hilo kwa muda ili kuonyesha nia njema licha ya athari mbaya iliyotokana na upunguzaji wa kamisheni kwenye biashara.
Hili lilifanyika ili kuunda fursa ya azimio la makubaliano ili kuendeleza sekta ya taxi mtandao nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye taarifa hiyo Meneja wa Bolt Ukanda wa Afrika Mashariki, Kenneth Micah, alisema “tunapenda kuwashukuru LATRA na mamlaka zinazohusika ambazo zimefanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kuwa kero zilizotolewa na wadau wa tasnia zinashughulikiwa, ili kuhakikisha hali ya mafanikio kwa wadau wote”.
Kwa kuzingatia kanuni mpya za LATRA kwa wahusika wa tasnia ya taxi mtandao, Bolt itafanya mabadiliko kwenye kamisheni pamoja na nauli kulingana na mwongozo mpya wa LATRA.
Bolt itaendelea kutoa huduma ya uhakika kwa mamia na maelfu ya watumiaji Tanzania Bara, ili waendelee kupata njia nafuu, salama na rahisi ya kuzunguka mjini.
Pia tutahakikisha kuwa maelfu ya madereva wanaoendesha kwenye jukwaa la Bolt nchini Tanzania, wanaendelea kupata fursa za mapato.
Bolt itaendelea kushirikiana zaidi na LATRA pamoja na wadau wengine wa tasnia hii, ili kuhakikisha ukuaji wa soko huria na zuri la huduma za usafiri wa taxi mtandao nchini Tanzania.