The House of Favourite Newspapers

Bombardier Ya Kwenda Bukoba Yakwama Mwanza

0

NDEGE ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) iliyoondoka saa 12:00 asubuhi Dar es Salaam kwenda Bukoba kupitia Mwanza, imekwama jijini Mwanza baada ya kupata hitilafu.

Kuharibika kwa ndege hiyo kumesababisha abiria waliokuwa wakielekea Bukoba kukwama hadi sasa bila kuelezwa hatima yao.

Akizungumza kwa simu, mmoja wa abiria ambaye alikuwa anaelekea kwenye msiba wa shemeji yake kutokea Mwanza, Muhiddin Khalid alisema alitakiwa kuripoti saa 12:15 asubuhi na walipanda ndege saa 2:15 asubuhi walitakiwa kufika Bukoba saa 3:15.

“Baada ya kupanda tulikaa muda mrefu ndani bila ndege kuondoka, baadaye tumeambiwa tushuke ndege mbovu, hivyo mpaka sasa saa 6:05 tupo hapa hatujui kinachoendelea tumeambulia kikombe cha chai,” alisema Khalid.

Meneja wa ATCL Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Theonestina Alchard amesema ni masuala ya kiufundi hivyo hawezi kuzungumzia zaidi kwa sababu yeye siyo msemaji wa kampuni.

Leave A Reply