The House of Favourite Newspapers

Itakuliza! Baba Aliyepata Ajali Ya Noah Na Familia Yake Asimulia Walivyosombwa Na Maji… – Video

0

Kufuatia familia ya Neiman Metili wa Ilboru mkoani Arusha kupata ajali mbaya na gari lao aina ya Toyota Noah walilokuwa wakisafiria kutokea Arusha kuelekea mkaoni Kilimanjaro kusombwa na maji maeneo ya Malula King’ori wilayani Arumeru na kusababisha vifo vya watoto watatu wa familia yake, baba huyo ambaye pia ndiye aliyekuwa dereva amefunguka.

Neiman anaeleza kuwa hakufanya kusudi kupitisha gari lile kwenye maji, bali gari hilo lilikuwa kwenye msafara wa magari mengi tu na gari za mbele yake zilipita ndiyo na yeye akaamua kupita, lakini ghafla hali ilibadilika na kusikia kishindo katika tairi za mbele na gari kusombwa na maji.

Aidha, baba huyo ameieleza Global TV kuwa baada ya kusombwa na maji yeye gari lilimtupa nje na wengine walibaki ndani ya gari hilo hata mauti ikawakuta japokuwa yeye aliokolewa na wasamaria wema kwani hajui kuogelea.

Leave A Reply