The House of Favourite Newspapers

Bondia Shaban Kaoneka Achangiwa Shilingi Milioni Moja na Shabiki wa Mandonga -Video

0

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Shaban Kaoneka leo ameweza kuchangiwa kiasi cha Shilingi milioni moja na mmoja kati ya mashabiki wa bondia Karim Mandonga kufuatia malalamiko yake juu ya kukosa bahati kama ilivyokuwa kwa Mandonga.

Kaoneka amechangiwa fedha hiyo leo Januari 10, 2023 na shabiki huyo ambaye amejimbulisha kama shabiki wa Mandonga katika kipindi cha Mapito kinachorushwa na +255 Global Radio na Global TV Online, ikiwa ni siku chache tangu aonekane Arusha katika Kanisa la Nabii mkuu GeorDavie.

Mtangazaji wa kipindi cha Mapito kinachorushwa na +255 Global Radio na Global TV Online,  Zari Adam (kulia) akimkabidhi Kaoneka kiasi cha Shilingi milioni moja.

Katika kipindi hicho kilichoruka mapema leo Jumatano, Kaoneka aliulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Zari Adam ataje matatizo yake ndiyo alisema anadaiwa kodi kiasi cha Sh 50,000 pamoja na kuomba kutafutiwa meneja ili aweze kufanya vizuri kwenye mapambano yake, hali iliyopelekea mtangazaji huyo kuanzisha mchango kwenye kipindi hicho kwa Kaoneka kutaja namba yake ya simu ambapo alipokea kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kodi ya mwaka mzima.

Baada ya kupokea kiasi hicho Kaoneka alimshukuru shabiki huyo ambaye alijitambulisha kama shabiki wa Mandonga bila ya kutaka kujulikana majina yake halisi.

Picha ndogo kulia Shaban Kaoneka akikabidhiwa kiasi cha Shilingi milioni moja na mtangazaji wa kipindi cha mapito mara baada ya kutoa kwenye simu yake.

Leave A Reply