The House of Favourite Newspapers

Bonge la Mtu Lenye ‘Maguvu’ na Mlo wa Kutisha

1

 

Hayat alivyo.

KWA kawaida, vibonge wengi, yaani watu wenye miili mikubwa hasa wanene, huchukuliwa kama watu wasio na nguvu na wavivu wa kuifanyia miili yao mazoezi, lakini kuna pia vibonge ambao ni watu wenye nguvu nyingi ambao wanaweza kumshangaza mtu yeyote kwa kuonyesha vipaji vya hali ya juu kwa kutumia ubonge wa miili yao.

 

2

…Akiwa na mashabiki wake.

Hivi sasa, mmoja wa watu wanaoaminika kuwa na nguvu zaidi duniani, ni mwanamme Arbab Khizer Hayat raia wa Pakistan aliye na uzito wa kilo 453.

3

Akivuta magari mawili kwa pamoja.

Mtu huyo ambaye kwa nchini Pakistan  ndiye mwenye nguvu zaidi, nguvu za mwili wake zimetokana kujengwa pia na chakula anachokula kila siku ambacho ni pamoja na kilo tatu za nyama, mayao 26 ‘anayojichana’ wakati wa kifungua kinywa na lita zaidi ya tano za maziwa.

4…Akivuta Trekta.

Vitu hivyo anavyokula, humzalishia mwilini kizio (kalori) cha joto litolewalo na chakula kifikiacho 10,000.

 

5

…Amembeba mtu juu kwa mkono.

“Sina masharti yoyote ya kiafya ambayo nimepewa na madaktari ili niyafuate na wala sijisikii vibaya kutokana na uzito wangu.  Hivyo ni lazima niendelee na hali hiyo iwapo ninataka kuwa bingwa wa dunia mwenye nguvu zaidi,” anasema Hayat ambaye alianza kufikiria kujiunga na mchezo wa kubeba uzito wangu alipokuwa bado mdogo.

Hivi sasa, kibonge huyo mwenye urefu wa mita 1.9 na umri wa miaka 25,  moja ya dhamira zake ni kuwa bingwa wa mashindano ya mieleka duniani.

Mamia ya watu wa eneo analoishi huenda nyumbani kwake na kupiga  picha na kibonge huyo.

“Watu wananipenda sana, lakini sitaki kuishia hapa tu; ninataka kuwa staa wa dunia,” anasema  na kuongeza kwamba pamoja na kwamba nchini Pakistan hakuna matarajio yenye matokeo chanya ya michezo ya watu wenye nguvu au kuinua uzito mkubwa, anategemea hali itabadilika na kuwa njema hivi karibuni.

KUTOKA MITANDAONI

 

SHINDA NYUMBA YA AWAMU YA PILI YATIKISA JIJI LA DR ES SALAAM.

Comments are closed.