The House of Favourite Newspapers

Bonge la Ngoma: Scopion Kings X Tresor (Official Video – Funu)

0

MASTAA wa kundi la muziki la Scopion Kings,  DJ Maphorisa na Kabza De Small kwa kushirikiana na mkali wa Afro Pop, Tresor kutoka Afrika Kusini, wameachia video ya kibao kinachokwenda kwa jina la Funu.

 

Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya kuachia singo hiyo mwishoni mwa mwaka jana, ambayo ni miongoni mwa nyimbo 14 zinazopatikana kwenye albamu yao mpya iitwayo ‘Rumble In the Jungle’.


Katika video hiyo iliyoongozwa na dairekta mkali, Kyle White inaonyesha kundi la vijana wa Kiafrika wakiwa katika jumba moja jijini Johannesburg, wakicheza na kufurahia tamaduni za Kiafrika.

 

Ubunifu wa jumba linaloonekana kama makazi ya wakoloni wa zamani na namna wanavyopaisha utamaduni wa Kiafrika, kwa pamoja vinaifanya video hiyo kutochosha.

Mastaa hao wakiwa kwenye wimbo huo, wanasikika wakitumia lugha za Kiingereza na Kiswahili – ambayo inazungumzwa na watu wengi hivi sasa ulimwenguni.

 

 

Wimbo wao wa kwanza walioutoa ‘Rumble In The Jungle’, uliwafanya Maphorisa and Kabza De Small wazidi kujiimarisha nchini Afrika Kusini wakiwa kama ma-DJ’s, walioipaisha staili ya Amapiano na kutangaza utamaduni wa Mwafrika duniani.

Na Mwandishi Wetu

Leave A Reply