The House of Favourite Newspapers

Bongo Movie Waongoza Zoezi la Kuchangia Damu

Wasanii wakipiga picha ya pamoja.

Chama cha Wanawake Watasnia ya Filamu Tanzania (CWTF) , leo wameongoza zoezi la uchangiaji wa damu katika Stendi ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar.

 

Wasanii na wananchi wengine wakichangia damu.

Akizungumza na GPL Mwenyekiti wa CWTF, Vanita Omary alisema kuwa, lengo la chama chao ni kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuchangia damu.

 

 

Wakijitokeza kuchangia damu.

“Leo WCTF tumezindua rasmi kampeni ya kuchangia damu na zoezi hili litafanyika kwa wiki nzima hadi Januari 11 kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya viunga vya Jiji la Dar, huku kilele cha zoezi hilo itakuwa ni Januari 13, 2018 katika Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini hapa.

 

Baaadhi ya bags zenye damu iliyotolewa na wasanii hao.

“Katika kuhitimisha zoezi hilo, kutakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo Upimaji wa Kansa ya Shingo ya Kizazi, matiti, Ushauri wa uzazi salama na upimaji wa virusi vya ukimwi na ushauri nasaha. ambavyo vitatolewa bure,” alisema Vanita.

 

Zoezi la kuchangia damu likiendelea.

Baadhi ya wasanii waliofika katika zoezi hilo ni Nikita, Recho Mwigoha, Badra, Sabrina, Adefina, Nandy wa Jumba, lucknessy, Ruby, Vivian, Dina, Miriama, Melania na wengineo, huku Msanii wa Filamu, Kupa akiwa ndiyo MC wa Shughuli hiyo. Zoezi hilo limeandaliwa na WCTF kwa kushirikiana na Damu Salama, Umati na Jhpiego.

 

Zoezi la kuhimiza uchangiaji damu likiendelea.

 

Wasanii katika picha ya pamoja.

 

 

Na Mwandishi Wetu/GPL

Comments are closed.