The House of Favourite Newspapers

Safari ya Mwisho ya Mpiga Picha Athumani Msengi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Dkt. Msengi msibani hapo.

MWILI wa  aliyekuwa mpigapicha wa magazeti ya serikali (TSN), Athumani Hamisi Msengi,  unatarajiwa  kuzikwa  leo Januari 5 mchana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam baaya dua iliyofanyika katika Msikiti Uliopo Sinza Madukani, Mtaa wa Namnani.

 

Msengi alifariki jana asubuhi katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Ndugu wa marehemu wakiwa wenye huzuni.

Msiba huo upo nyumbani kwa marehemu Sinza-Madukani,  Mtaa wa Weruweru, Nyumba namba  26 ambapo mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa Serikali walioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul makonda, wanahabri, ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza kwa ajili ya kumsindikiza Msengi katika safari yake ya mwisho.

Jeneza lenye mwili likipelekwa msikitini.

 

Mwili ukifikishwa msikitini.

 

Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa nyumbani kwa marehemu Sinza Madukani.

 

Msikiti ambapo mwili huo umefanyiwa dua kabla ya mazishi.

 

Safari ya msikitini.

 

Mashehe wakiomba dua.

 

NA RICHARD BUKOS | GPL

Babu Seya, Papii Kocha Waingia Studio Kurekodi, Watazame

Comments are closed.