The House of Favourite Newspapers

MAJI TAKA DAR, MWAROBAINI WAPATIKANA

Meneja wa Manispaa ya Kinondoni, Ramadhani Mabula (aliyesimama) akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam sambamba na maonyesho.

KAMPUNI ya Borda ya jijini Dar es Salaam imeanzisha huduma ya utunzaji wa mazingiya inayotambulika kama  ‘Choo Rafiki’  yenye lengo la kupambana na utiririshaji maji taka hovyo.

Wawakilishi wa kampuni ya Borda wakisikiliza kwa makini mpango-kazi wa huduma ya Choo Rafiki.

Meneja wa Manispaa Kinondoni, Ramadhani Mabula, amesema programu hiyo ya Choo Rafiki inalenga  kuzuia utiririshaji wa maji taka mitaani kutoka majumbani ambapo itatoza Shilingi 20,000 kwa kila kaya.

Wafanyakazi wa Borda ngazi ya juu wakipata maelekezo kutoka kwa wataalam wa huduma hiyo ya namna ya matumizi ya chemba za kukusanyia maji-taka.

Comments are closed.